KUTANA NA MWANZILISHI NDUGU HUSSEIN MSHUNGA

 Hussein Mshunga ambaye ni Mwanzilishi wa CHILD PSYCHOLOGIST TANZANIA 

(Brela Reg. No. 497719), ana  ndoto ya kuhakikisha huduma za kisaikolojia zinawafikia watoto wote Nchini Tanzania.

 Ana shahada ya Elimu katika Saikolojia (Bed Psychology (Hons) kutoka Chuo kikuu cha Da es salaam (UDSM), Pia ni Muasisi wa Tanzania Autism Resource Centre Taasisi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na kusaidia watoto wanaoishi na Usonji kuongeza uwezo wao maishani kupitia Uchechemuzi (advocacy) na utoaji wa huduma katika elimu, tiba na uwezeshaji wa walezi ,wazazi na wataalamu wanaowahudumia. 

Pia ni mnufaika wa mradi wa Learning Journey into Leadership for Young Changemakers ulioanzishwa na Swiss centre of competence for international cooperation, na kudhaminiwa na  Fondation Botnar ya nchini Uswisi.

Hussein Mshunga Bed.Psychology (Hons) UDSM, Associate Member Tanzanian Psychological Association (TAPA)


Saikolojia ya watoto ni moja ya matawi mengi ya saikolojia. Tawi hili linazingatia akili, ukuzi wa mfumo wa fahamu na tabia ya watoto kutoka kipindi cha  ukuaji wa ujauzito mpaka kuvuka umri wa  balehe. 

Baada ya kufanya kazi hii ya kutoa huduma za kisaikolojia kwa watoto kwa muda unaozidi nusu muongo sasa, Hussein Mshunga ameweza kuwafikia mamia ya watoto hapa nchini Tanzania kupitia taasisi aliyoianzisha na wakati mwingine akishirikiana na mashirika mengine.

 Pamoja na jitihada zote,  ukweli ni kwamba wale wanaopata huduma hizo kwa urahisi ni watoto wanaotoka katika familia zenye kipato cha kati na cha juu.

 Hivyo kundi kubwa lingine la watoto linabaki bila kupokea huduma hizo ifaavyo na kwa wakati unafofaa. Watoto hawa wanasahaulika kana kwamba wao hawapitii changamoto zinazohitaji msaada wa wataalamu wa kisaikolojia kama yeye.

Hussein Mshunga akiwa katika moja ya shughuli zake za kila siku


 Kuhakikisha maono yake yanatimia amekuja na  mikakati kadhaa,

1.   1. Kufanya uchechemuzi  kwa kuanzia katika ngazi ya chini kabisa (grass root level) mpaka ngazi ya sera ili kutoa elimu kwa umma na kuchagiza mabadiliko katika mfumo wa utoaji wa huduma hizi za kisaikolojia

2.   2. Kushirikiana na sekta ya umma, sekta binafsi ,taasisi mbalimbali zisizo kiserikali katika  kuandaa ,kutekeleza na Kuripoti shughuli mbali mbali zitakazofanyika ili Kupunguza  pengo hili la utoaji wa huduma  ya afya ya akili kwa watoto.

 

Ukiwa mdau na sehemu ya jamii bila shaka una maoni ambayo yatasaidia kuifikia azma hiyo , basi usisite kuandika maoni yako hapa chini, au kutuandikia kupitia mailto:childpsychologisttanzania@gmail.com


 

 

 


Comments

  1. Hongera sana! Jitihada zako zimekuwa na mchango mkubwa Mara zote. Mapambano yaendelee!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante kwa kutumia muda wako kusoma chapisho letu, tunashukuru na kuthamini mchango wako

      Delete
  2. Hongera sana tena sana, watoto wenye usonji wamekuwa wakisaulika sana hapa Tanzania, kupitia jitihada zako, naamini itafika mahal watanzania wengi tutakuwa na uelewa na msaada katika hili tatizo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante kwa kutumia muda wako kusoma chapisho letu, tunashukuru na kuthamini mchango wako

      Delete

Post a Comment

Popular posts from this blog

CHILD PSYCHOLOGIST TANZANIA

JEAN PIAGET - THE FOUNDING FATHER OF MODERN CHILD PSYCHOLOGY